JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Habari

WOISO AVUTIWA NA HUDUMA ZA POSTA


Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni ya bidhaa za ngozi, (WOISO Leather Products Tanzania), Bw. Keneth H. Woiso, ametembelea banda la Shirika la Posta Tanzania katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo amepata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.



Akiwa katika banda hilo, Bw. Woiso, alipewa maelezo kuhusu huduma za usafirishaji wa vifurushi, mizigo na nyaraka mbalimbali zinazokidhi mahitaji ya wananchi na wafanyabiashara.



Baada ya kutembelea banda hilo, Bw. Woiso alionyesha kuvutiwa na ubora wa huduma zinazotolewa na Shirika la Posta Tanzania, akibainisha kuwa huduma hizo zina mchango mkubwa katika kurahisisha shughuli za biashara, kuimarisha huduma za ugavi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.



Imeandaliwa na;
Kitengo Cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania


© SHIRIKA LA POSTA TANZANIA